The State University Of Zanzibar

Uongozi wa SUZA na KIST Wajadili Kuimarisha Ushirikiano wa Kitaaluma na Udahili Zanzibar

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA Prof. Abdi Talib Abdlalla amepokea ugeni kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST) kwa kufanya mazunguzo ya Kitaaluma.

Ugeni huo ulioongozwa na Kaimu Naibu Mkuu wa Taasisi ya Taaluma, Utafiti, Ubunifu na Ushauri Elekezi Dkt. Zuhura Juma Ali pamoja na Mkuu wa Divisheni ya Udahili na Usajili Ndugu Amour Kombo Hassan.

Mazungumzo hayo yalijikita katika kuboresha utoaji wa taarifa za Udahili kwa wanafunzi waliomaliza ngazi ya Stashahada kutoka KIST na kuendelea na masomo ngazi ya Shahada katika Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA.

Aidha Prof. Abdi aliwaomba KIST kufikiria juu ya kuwepo kwa Hati ya Makubaliano (MOU) kati ya SUZA na KIST ili kutengeneza ushirikiano wa kitaaluma.

Sambamba na hayo ugeni huo uliendelea kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Shahada za Awali SUZA Dkt. Khamis Haji Salum ili kuangalia namna bora ya utoaji elimu, kutatua changamoto za Udahili kwa wanafunzi wa KIST ili kujiunga katika fani mbalimbali za Sayansi na Teknolojia kwa ngazi ya Shahada.

Mazungumzo hayo yalifanyika tarehe 26 Mei 2026, Makao Makao SUZA Tunguu Zanzibar.

Picha na Kitengo cha Uhusiano na Masoko SUZA.