The State University Of Zanzibar

SUZA ANTHEM

Verse 1

MOLA USO MSHIRIKA

YARABI MOLA MUWEZA

UKIPE ZAKO BARAKA

CHUO KIKUU CHA SUZA

ZANZIBAR KUIMARIKA

KOTE KIWE CHATAJIKA

SUZA KICHOCHEO CHA MABADILIKO KWA JAMII

Verse 2

FANI ZOTE KWA UPEO

NA TAFITI KUFANYIKA

UMAHIRI, UZALENDO

CHUO KINAZINGATIA

KUFUNDISHA KWA VITENDO

WAHITIMU KUBOBEA

SUZA KICHOCHEO CHA MABADILIKO KWA JAMII

Verse 3

WABARIKI VIONGOZI

UTUMISHI ULO BORA

NA WOTE WAFANYAKAZI

TAALUMA KUINUA

SUZA YETU KUIENZI

MBELE KUENDELEA

SUZA KICHOCHEO CHA MABADILIKO KWA JAMII