




Uongozi wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA) umekutana na uongozi wa Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar (SUZA). Lengo kuu la mkutano huo ni kuanzisha mashirikiano ikiwemo kuwa na Hatinya Mashirikiano na uanzishaji wa Klabu ya ya Wanafunzi ya Wakaguzi wa Ndani.
Ujumbe huo umeongozwa na Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo Ndg. Seif Hassan walipokelewa na Dkt. Idd Salum Haji Mkuu wa Skuli ya Biashara SUZA kwa niaba ya Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Fedha, Mipango na Utawala Prof. Salum Seif Salum.
Akizungumza kwa niaba ya uongozi wa Chuo Dkt. Idd amesema kuwa ujio umefika kwa wakati muafaka na Chuo kipo tayari kuwa na mashirikiano na IIA, huku Mtendaji Mkuu Ndg. Seif akisema kuwa watawasilisha rasimu ya mashirikiano siku chache zijazo.
Kikao hicho kilifanyika tarehe 19/05/2026, Kampasi ya Tunguu.