Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Abdi Talib Abdalla amesema taaluma ya Akili Unde kwa wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA itasaidia wahadhiri kukuza na kurahisisha taaluma zao.
Akifungua Warsha ya Mafunzo ya Taaluma ya Akili Unde iliyotayarishwa na Kituo cha Kimataifa cha Taaluma za Kiswahili na Uenezi (GCKSA) katika Skuli ya Kiswahili na Lugha za Kigeni Vuga Mkoa wa Mjini Magharibi.
Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Utafiti wa Mafunzo ya Uzamili na Ushauri katika Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Dkt Miza Ali Kombo kwa niaba ya Kaimu Makamu Mkuu Mkuu SUZA.
Prof Abdi amesema kuwa warsha hiyo itawajenga wahadhiri na wanafunzi wa uzamili katika matumizi ya teknolojia ambayo yatawasaidia na kuwarahisishia kukuza taaluma zao.
Aidha amefafanua kuwa mafunzo hayo yatatoa msingi imara wa kuelewa na kutumia zana za Akili Unde (AI) katika mazingira ya kitaaluma na kielimu.
Mafunzo hayo yataendeshwa kwa kipindi cha siku mbili, Mei 13 hadi 14 mwaka huu.
