The State University Of Zanzibar

Uongozi wa SUZA Wapokea Michoro ya Awali ya Mradi wa BADEA Kampasi ya Tunguu

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar umepokea wasilisho la michoro ya awali ya miundombinu mbalimbali inayotarajiwa kujengwa kupitia mradi wa BADEA kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutoka kwa mshauri elekezi Y&P Architects Co. Ltd.

Miongoni mwa miundombinu hiyo ni Jengo la Utawala, Jengo la Skuli ya Elimu na Lugha, jengo la Huduma za Wanafunzi, nyumba za wafanyakazi na miundombinu ya michezo ikiwemo mpira wa miguu, kikapu na wavu. Miundombinu yote hii inatarajiwa kujengwa Kampasi ya Tunguu.

Uwasilishwaji huo umefanyika tarehe 6Mei, 2026 katika Kampasi ya Tunguu.

Mradi huu wenye thamani ya Bilioni 26 ya ujenzi ambapo ukikamilika unatarajiwa kusaidia kuongeza idadi ya udahili wa wanafunzi, kuongeza ubora wa Elimu , aidha utasaidia kuongeza ajira kwa wananchi na Jamii inayozunguuka maeneo ya Chuo.