The State University Of Zanzibar

SUZA, ZJNU Kuendeleza Mashirikiano ya Kitaaluma

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Cha Zanzibar SUZA, Prof. Abdi Talib Abdalla amewasisitiza wanafunzi wa chuo hicho kuchgangamkia fursa ya kujifunza Lugha ya Kichina kutokana na kua na fursa nyingi zinazo patikana katika lugha hiyo

Akizungumza kwa Niaba yake, Mkuu wa Skuli ya Elimu SUZA Dkt. Said Khamis Juma Wakati wa hafla ya Kukabidhi Tuzo kwa wanafunzi walio fanya vizuri katika darasa la kichina kwa mwaka 2025, hafla ilifanyika tarehe 3 Januari,2025, katika ukumbi wa Utulivu Kampasi ya Utalii Maruhubi, alisema kuwa kujifunza kichina si kujifunza lugha pekee bali ni kufungua fursa mpya za kimataifa haswa za kiteknolojia na kidiplomasia

Alisema Urafiki uliopo kati ya SUZA na Chuo cha Zhejiang Normal University (ZJNU ) umefungua fursa pana kwa wanafunzi wanaotaka kujifunza lugha hiyo kutokana na kuwepo ongezeko kubwa la wanafunzi kutoka SUZA kupenda kujifunza lugha kichina

Aidha aliwataka wanafunzi walio fanya vizuri na ambao hawajafanikiwa kupata tuzo hizo zinazotolewa na ubalozi mdogo wa China unao fanya kazi zake Zanzibar Kuongeza bidii na ari ya kujifunza lugha hiyo ili kutanuwa fursa zaidi za ajira na kimasomo

Balozi mdogo wa China anae fanya kazi zake Zanzibar Bw. Li Qianhua aliipongeza SUZA pamoja na ZJNU kwa kuanzisha Somo la lugha ya kichina visiwani Zanzibar ambapo ambalo limesaidia wanafunzi hao kupata fursa mbali mbali nchini china zikiwemo za masomo

Alieleza kuwa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi kutoka Tanzania ni moja ya hatua muhimu za kukuza urafiki uliopo kati ya China na Tanzania ambapo darasa hilo tangu kuanzishwa kwake limeshatoa wanafunzi Wanne Walio fadhiliwa na serikali ya china kwenda kujifunza nchini China.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa darasa hilo Tanzania kutoka SUZA, Prof. Moh’d Makame Haji alihimiza mashirikiano kati ya SUZA na ZJNU kutokana na kusaidia wanafunzi kutoka Tanzania kujifunza lugha hiyo kwa karibu na kwa urahisi zaidi

Nae Mkuu wa Darasa hilo Zanzibar Bi. Qian Ming Ming alisema kua SUZA kwa kipindi cha miaka Mitatu imetoa mashirikiano makubwa ambapo kichina kimekua kikifundishwa katika Kampasi Tatu, Habari kilimani, Utalii Maruhubi na kampasi ya Ualimu Betrasi ambapo kwa sasa imehamishiwa Kampasi Kuu ya Tunguu.

Tuzo hizo Hutolewa kila Mwaka ambapo kwa Mwaka huu Jumla ya wanafunzi 43, wamekabidhiwa Tuzo maalum, kati ya hao wanafunzi Watatu wameibuka wanafunzi bora kati ya wanafunzi wote.