
CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR (SUZA)
Sanduku la Posta 146, Zanzibar- Tanzania
Simu:+255 24 2233337/773333167 Nukushi:+255 24 2233337
Tovuti: http://www.suza.ac.tz Barua pepe: vc@suza.ac.tz
SALAMU ZA PONGEZI

Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Baraza la Chuo, Menejimenti, na Wanajumuiya wote wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) wanatoa salamu za dhati za pongezi kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuchaguliwa kwa kishindo kuongoza taifa katika kipindi cha pili cha Awamu ya Sita kupitia Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 29 Oktoba, 2025.
Kuchaguliwa kwako kwa kura nyingi kunadhihirisha kwa uwazi kukubalika kwa juhudi zako thabiti katika kuendeleza maendeleo ya wananchi na kuijenga nchi kwa misingi ya uwajibikaji, ushirikishwaji na dira ya kitaifa. Mafanikio haya yanadhihirika kupitia utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati kama vile ujenzi wa Reli ya Kisasa, Bwawa la Mwalimu Nyerere, vyuo vya elimu ya juu, hospitali, vituo vya afya, barabara, meli, pamoja na kuwawezesha wavuvi, wakulima na wafugaji kufanya shughuli zao kwa mbinu za kisasa. Aidha, umefanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu kuanzia ngazi ya awali hadi elimu ya juu, sambamba na kusimamia kwa ufanisi amani, utulivu na mshikamano wa kitaifa.
Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kinaendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuijenga nchi kwa kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya elimu ya juu, tafiti zenye tija, na utoaji wa ushauri wa kitaalamu, ili kuchochea mabadiliko chanya ya kiuchumi na kijamii kwa manufaa ya taifa.
Aidha, SUZA itaendelea kuwa mshirika madhubuti wa Serikali katika kutekeleza kwa bidii Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa lengo la kuimarisha juhudi za maendeleo ya Tanzania na kuendeleza ustawi wa wananchi wake katika nyanja zote za kijamii, kiuchumi, kisayansi, na kielimu.
Kwa taarifa zaidi kuhusu Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar tembelea tovuti
Mawasiliano rasmi na Chuo yafanywe kupitia kwa:
Makamu Mkuu wa Chuo
Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar
Sanduku la Posta 146
Zanzibar, Tanzania
Barua pepe: vc@suza.ac.tz
Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ni Kichocheo cha Maendeleo ya Jamii.