
CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR (SUZA)
Sanduku la Posta 146, Zanzibar- Tanzania
Simu:+255 24 2233337/773333167 Nukushi:+255 24 2233337
Tovuti: http://www.suza.ac.tz Barua pepe: vc@suza.ac.tz
SALAMU ZA PONGEZI

Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Baraza la Chuo, Menejimenti na Wanajumuiya wote wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) wanatoa salamu za dhati za pongezi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais Mteule wa Zanzibar awamu ya nane kwa kuchaguliwa kwa muhula pili katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa tarehe 29 Oktoba, 2025 kwenye nafasi ya urais.
Kuchaguliwa kwako kwa mara ya pili kunadhihirisha kukubalika kwa juhudi zako za kuleta maendeleo ya wananchi kwa kuijenga nchi na kusimamia miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu wa Skuli za ghorofa, Vyuo, Hospitali, vituo vya afya, barabara, masoko, kuwawezesha kifedha wajasiriamali, kuimarisha uwajibikaji kwa kupiga vita rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma, pamoja na kusimamia amani na utulivu nchini.
Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kinaendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuijenga nchi kwa kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya elimu ya juu, tafiti zenye tija, na utoaji wa ushauri wa kitaalamu, ili kuchochea mabadiliko chanya ya kiuchumi na kijamii kwa manufaa ya taifa.
Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kitaendelea kuwa mshirika thabiti katika kutekeleza kwa bidii Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, kwa lengo la kuimarisha juhudi za maendeleo ya Zanzibar na ustawi wa wananchi wake katika nyanja zote za kijamii, kiuchumi, kisayansi na kielimu.
Kwa taarifa zaidi kuhusu Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar tembelea tovuti
Mawasiliano rasmi na Chuo yafanywe kupitia kwa:
Makamu Mkuu wa Chuo
Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar
Sanduku la Posta 146
Zanzibar, Tanzania
Barua pepe: vc@suza.ac.tz
Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ni Kichocheo cha Maendeleo ya Jamii.