The State University Of Zanzibar

Prof Moh’d Makame Haji amehudhuria kikao cha Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Prof Moh’d Makame Haji amehudhuria kikao cha Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kilichojadili Hutuba ya Bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa mwaka wa fedha 2025/2026 iliyowasilishwa tarehe 27 Mei, 2025 katika Ukumbi wa Bunge, Dodoma kwa mualiko wa Mhe. Waziri wa Dkt. Dorothy Gwajima na Naibu wake Mhe. Mwanaidi Ali Khamis.

Ushiriki wa SUZA katika tukio hili muhimu unaakisi dhamira ya chuo katika kuimarisha usawa wa kijinsia, kulinda haki za jamii, na kuboresha ustawi wa wanafunzi na wafanyakazi wake. Kupitia program zake za elimu, utafiti na huduma kwa jamii, SUZA imeendelea kutekeleza jitihada mbalimbali zinazolenga kuleta mabadiliko chanya, ikiwa ni pamoja na:

1.⁠ ⁠Kuaanzisha madawati ya jinsia yanayotoa msaada kwa wanafunzi na wafanyakazi kuhusu masuala yanayohusiana na usawa wa kijinsia, haki za wanawake, na uzuiaji wa ukatili wa kijinsia. Madawati haya yanatoa fursa ya kupata ushauri nasaha, ulinzi wa haki, na mazingira salama kwa wote.

2.⁠ ⁠Chuo kimetengeneza sera na programu maalum zinazolenga kusaidia makundi maalumu, ikiwa ni pamoja na watu wenye ulemavu, wanawake katika elimu ya juu, na wanafunzi kutoka mazingira magumu. Kupitia ufadhili wa masomo, mafunzo ya stadi za maisha, na fursa za masomo ya jinsia na elimu mjumuisho. SUZA inaendeleza jitihada za kuhakikisha kila mtu anapata nafasi sawa ya kujifunza na kujiendeleza.

3.⁠ ⁠Kuandaa mijadala na semina zinazohamasisha usawa wa kijinsia, pamoja na kuimarisha sera zinazoendeleza fursa sawa kwa wote.

4.⁠ ⁠SUZA pia inashirikiana na wadau mbalimbali katika kukuza uelewa na utekelezaji wa sera zinazohakikisha haki za wanafunzi na wafanyakazi zinalindwa.

5.⁠ ⁠Kuendeleza programu za afya na ustawi zinazolenga kuboresha mazingira ya kujifunza na kufanya kazi ndani ya chuo.