Dkt. Hashim Hamza Chande, ameonesha kutoridhishwa na uzembe wa baadhi ya watendaji wa Idara ya Manunuzi na Ugavi kufuatia ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi chuoni.
Dkt. Chande alitoa kauli hiyo baada ya kukagua baadhi ya maeneo ya Skuli ya Afya yaliyoonekana kutoendelezwa. Alielezwa kuwa ucheleweshaji huo unasababishwa na changamoto za manunuzi na urasimu wa kiutendaji.
Ziara hiyo ni sehemu ya ukaguzi wa Kampasi zote zilizo chini ya SUZA, Unguja na Pemba, kwa lengo la kufuatilia maendeleo na kubaini changamoto zilizopo.
Amekitaka Kitengo cha Manunuzi kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha taratibu za ununuzi zinatekelezwa kwa wakati ili kuimarisha utoaji wa huduma na kuepusha hasara kwa Chuo.
https://www.instagram.com/reel/DKMJ6fRoSgs/?igsh=NnByeWFyNDY4emJ4