The State University Of Zanzibar

Ujenzi wa jengo la Skuli ya Kilimo (Agriculture Building)

Ujenzi wa jengo la Skuli ya Kilimo (Agriculture Building) na la Maabara (Laboratory Complex) wa mradi wa Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi (HEET) umefikia asilimia 33 hadi mwezi huu wa tano.

Taarifa hiyo imetolewa leo katika kikao cha tathmini ya ujenzi (Site Meeting) kimefanyika leo tarehe 28/05/2025 Makao makuu ya Chuo Tunguu.

Aidha, kikao kimeshirikisha watendaji wa mradi wa HEET SUZA wakiongozwa na Mratibu wa mradi huo SUZA Dkt. Hashim Hamza Chande, Kampuni ya ujenzi ya Mohamed Builder pamoja na Mshauri Elekezi ARQES.