The State University Of Zanzibar

Prof. Moh’d Makame Haji ashiriki Mkutano Mkuu wa Nne wa Chama cha Maafisa Rasilimaliwatu na Utawala wa mwaka 2025

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, Prof. Moh’d Makame Haji, ambae pia ni Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Chama cha Maafisa Rasilimaliwatu na Utawala wa mwaka 2025 alishiriki kikamilifu katika Mkutano Mkuu wa Nne wa Chama cha Maafisa Rasilimaliwatu na Utawala wa mwaka 2025 (4th Annual National Conference – 2025) uliofanyika kuanzia tarehe 20 – 22 Mei 2025 katika Hoteli ya New Amaan, Zanzibar, ambao ulikuwa na kaulimbiu kuu “Enhancing Human Resource Capacity and Professional Standards in Tanzania.”

Mkutano huo uliofunguliwa na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa BAraza la Mapinduzi, Mhe. Dr. Hussein Ali Mwinyi, ulihudhuriwa na maafisa rasilimaliwatu na autawala wa taasisi za umma na binafsi kutoka Tanzania.


Katika kongamano hilo, Prof. Makame alishiriki pia kama mchangia mada kwenye mjadala wa wazi, akielezea kwa kina jinsi sera za rasilimali watu (HR policies) na sheria za kazi zinavyoweza kusaidia au kuzuia juhudi za kujenga uwezo na taaluma miongoni mwa wataalamu wa sekta mbalimbali. Mjadala huo uliangazia changamoto zinazokumba utekelezaji wa sera hizo, huku Prof. Makame akitoa mtazamo wa kitaalamu juu ya mbinu bora za kuhakikisha sheria na sera zinakuwa chachu ya maendeleo badala ya vikwazo.

Mjadala huo ulitanguliwa na neon kuu kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi akitoa uzoefu wake wa maswala mbalimbali yahusuyo wajibu wa maafisa rasilimali watu na utawala pamoja na kuainisha changamoto zake na kusisitiza kuimarisha utendaji kwa kuimarisha kada hio kuendana na vigezo vinavyohitajika.


Mkutano huu uliwaleta pamoja viongozi wa sekta za umma na binafsi, wataalamu wa rasilimali watu, pamoja na wadau wengine muhimu katika mchakato wa kuboresha nguvu kazi na viwango vya taaluma nchini Tanzania. Ushiriki wa Prof. Moh’d Makame Haji uliimarisha zaidi mijadala yenye tija kuhusu mustakabali wa taaluma ya rasilimali watu na umuhimu wa mfumo bora wa sera za kazi kwa maendeleo ya taifa.