The State University Of Zanzibar

‎SUZA Yapokea Wageni kutoka Chuo Kikuu cha New York na UNICEF

‎‎Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimepokea wageni kutoka Chuo Kikuu cha New York (NYU) cha Marekani pamoja na wajumbe kutoka UNICEF katika ziara ya kielimu iliyolenga kujifunza na kubadilishana uzoefu.

‎Ziara hiyo imehusisha wanafunzi na wahadhiri kutoka NYU ambao walipata fursa ya kujifunza kuhusu historia, uchumi wa kisiasa, utawala na usalama wa Tanzania na Zanzibar. Mada mbalimbali pia zilijadili maendeleo ya uchumi na sekta ya elimu Zanzibar.

‎Wanafunzi walionesha shauku kubwa ya kujifunza kwa kushiriki kikamilifu katika mijadala na kuuliza maswali mengi yaliyochangia kuongeza uelewa kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Zanzibar.

‎Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa WASTEX Lab wa SUZA, ukiwa sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika elimu, utafiti na kubadilishana maarifa.

‎#OfficialSUZA #SUZA #Zanzibar #Elimu #UshirikianoWaKimataifa #NYU #UNICEF #HigherEducation