Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kinaendelea kujivunia mafanikio ya wataalamu wake, ambapo mtangazaji wa kipindi cha “Ifahamu Lugha Yako” kinachorushwa kupitia Radio Habari FM ya SUZA, ametunukiwa Tuzo ya Mtangazaji Chipukizi wa Vipindi vya Kiswahili Zanzibar.
Tuzo hiyo imetolewa katika Kongamano la 5 la Idhaa za Kiswahili Duniani 2026 lililofanyika jijini Arusha, likiwakutanisha wadau mbalimbali wa lugha ya Kiswahili kutoka ndani na nje ya nchi.
Kongamano hilo lilifunguliwa rasmi tarehe 24 Machi 2026 na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla, katika Ukumbi wa Kimataifa wa AICC, na kufungwa tarehe 26 Machi 2026 na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi BAKITA, Profesa Martin Mhando.
Mafanikio haya ni kielelezo cha juhudi, ubunifu na mchango mkubwa wa SUZA katika kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili kimataifa. Tunampongeza sana mshindi wetu na kumtakia mafanikio zaidi katika safari yake ya taaluma na utangazaji. 🌟