Naibu Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Hamad Hassan Chande amezindua mfumo wa wahitimu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) utakaokuwa na taarifa zao kuanzia mwaka 2002.
Mhe.Chande ambaye ni msajiliwa namba moja wa mfumo huo, alifyatua kitufe kuashiria uzinduzi huo na taarifa zake kuonekana.
Akitoa maelezo yanayohusu mfumo huo,a Mtaalau wa masuala ya mifumo, Ndg. Masoud Mmanga Hamad alisema mfumo utaanza kutembelewa na wahitimu kuanzia mwezi Januari 2025 ambapo taarifa zote za wahitimu zitapatikana.
Aliongeza kuwa wapo wahitimu walioko nje ya nchi na wanafanya mambo makubwa ya kutambuliwa pia taarifa zao zitasomwa kwenye mfumo huo.