










Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kwa kushirikiana na wataalamu kutoka nyanja mbali mbali za Mtandao wa Vitu (internet of Things- IoT) wamejadiliana maeneo ya ushirikiano wa kitaaluma ili kuimarisha utafiti wa elimu ya fani kadhaa kwa pamoja hapa Zanzibar.
Mkutano wa siku mbili ulijadili masuala ya kilimo,, ukusanyaji data, afya ya binadamu na wanayama, afya ya mazingira, Akili Mnemba, mabadiliko ya tabia nchi na masuala ya mlo kamili, uchumi wa buluu ambayo yameleta hamasa kubwa kwa wataalamu hao kwa kuonesha hamu ya kushirikiana kwa kuzipa msukumo sekta hizo.
Ujumbe huo uliojumuisha maprofesa 13 sambamba na wataalamu uliongozwa na Cristina Miceli, kutoka Chuo Kikuu cha Camerino cha Italia alielezea kufurahishwa kwake na mjadala huo na kutoa miongozo kwa maeneo ambayo hawataweza kushirikiana na SUZA kwa kuwaelekeza kwenye taasisi ambazo wanaweza kushirikiana nao.
Aidha, ameeleza kuwa UNICAM iko tayari kushirikiana na SUZA katika uchapishaji wa majarida kwani yatatoa fursa kwa wadau wengi zaidikufuatilia masuala ya SUZA kupitia majarida hayo.
Alifahamisha kuwa uhusiano wa SUZA na UNICAM ni wa muda mrefu na wamekuwa wakifanya kazi vyema katika masuala ya utafiti.
Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar (SUZA) Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Salum Seif Salum alielezea kuridhishwa kwake na na ziara ya wataalamu hao kwani itazidi kutanua wigo wa utekelezaji wa jukumu la kuimarisha eneo kufanya tafiti.
Alieleza kuwa matokeo ya mkutano huu yatazidi kuwatengeneza wanafunzi wa Stashahada na Uzamivu kuwa wabobezi katika fani wanazochukua.
Mkutano huo wa kitaaluma uliofanyika kampasi ya SUZA Maruhubi tarehe 15/01/2029 umewashirikisha wadau wa masuala ya tafiti, wanafunzi na wakuu wa Skuliza SUZA.