The State University Of Zanzibar

Wizara ya afya,SUZA, kuja na muarubaini wa maradhi ya kina mama Zanzibar

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Mngereza Mzee Miraji amesema Zanzibar inampango wa kujenga kituo cha kimataifa cha maradhi ya kansa kitakacho wezesha wagonjwa wa maradhi hayo kutibiwa hapa nchini.

Akifungua mkutao wa Tano wa Jumuiya ya African Woman Health, Uliofannyika Tarehe 16/01/2026, Dkt. Mngereza Alisema kupitia mkutano huo wamejadili namna bora ya kutokomeza maradhi yanayo wasumbua kinamama ikiwemo kansa,vifo vya mama na mtoto na maradhi mengine sugu ya kinamama.

Alieleza kuwa Serikali ya awamu ya nane iliyo chini ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ilifanya jitihada kubwa ya kuboresha sekta hiyo muhimu katika vifaa tiba,majengo ya kisasa, huduma za kidijitali ( CT SCAN, X RAY,ULTRA SOUND ) na kuongeza wataalamu wenye uwezo wa hali ya juu ishara inayo onesha uwajibikaji na usikivu wa serikali hiyo kwa watu wake.

Aliongeza kuwa kupitia mkutano huo wa siku mbili, wataalamu wa ndani wanapaswa kujifunza,kutengeneza mashirikiano na wataalamu kutoka nje pamoja na kutafuta muarubaini wa matatizo yanayo wasumbua kinamama.

Aidha alitumiya fursa hiyo kuwapongeza waandalizi wa mkutano huo kuichagua Zanzibar kuendesha mkutano huo na kuahidi kutoa mashirikiano ya hali ya juu kwa taasisi hiyo

Kwa upande wake Mkurugenzi kinga na elimu na afya Zanzibar, Dkt. Salum Slim Aliuweleza ujumbe wa mkutano huo kuwa Wizara ya Afya Zanzibar itahakikisha inapunguza vifo vya mama vinavosababisha na sababu tofauti zikiwemo vifo vya uzazi,maradhi ya kansa na malaria.

Alieleza kuwa kwa asilimia 60 vifo hivyo vinaweza kuzuilika kutokana na kuwa na miondombinu ya kutosha, huku kwa asilimia kubwa maradhi ya malaria yakiwa tayari yamedhibitiwa.

Nae Mkuu wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Dkt. Salma Abdi Mahmoud alisema SUZA kupitia Skuli yake ya Afya imeungana na wataalamu tofauti kujadili namna ya kusaidia kinamama katika Nyanja mbali mbali za kimatibabu

Dkt. Salma ambae pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama na kizazi, Alieleza kuwa SUZA imefanya mazungumzo na wataalamu kutoka Abu Dhabi na Marekani kuona namna ya kuwasaidia wataalamu na wanafunzi wa SUZA kupata taaluma zaidi ya magonjwa hayo, suala litakalo saidia kupatikana kwa wataalamu wengi wa ndani wa maradhi hayo nchni.

Aidha Dkt. Salma aliipongeza wizara ya Afya kwa kuboresha huduma za dharura za mama na mtoto hatua iliyo saidia kupunguza vifo na magonjwa ya kudumu.

Mkutanao huo ulio jumuisha wataalamu na watafiti wa afya, madakatari bingwa na Wanafunzi ni watano kufanyika tangu kuundwa kwa jumuiya hiyo na wapili kufanyika Tanzania ambapo awamu hii mefanyika visiwani Zanzibar na unatarajiwa kutamatika tarehe 17/01/2026.