The State University Of Zanzibar

SUZA yachangia kuanzishwa kituo cha Utafiti JWTZ

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Prof. Moh’d Makame Haji amesema analishukuru Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kuwashirikisha kuwa sehemu ya kuchangia andiko la kuanzishwa kwa Kituo kikubwa cha Tafiti cha Jeshi hili.
Hayo aliyasema katika makao makuu ya SUZA huko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja wakati akizungumza na ujumbe wa maofisa kutoka Jeshi la Wananchi tarehe 17/12/2024, Prof. Haji alisema SUZA ina uzoefu katika kuendesha tafiti kwa kushirikiana na vyuo mbali mbali vya Tanzania na taasisi za kimataifa.
Alifafanua miongoni mwa tafiti zilizowahi kufanywa ni kama vile zinazohusiana na ukuaji wa lugha ya Kiswahili, sayansi ya bahari, na nyegine zinazowashirikisha jamii ambazo zinatoa suluhisho la changamoto zinazowakabili wanajamii hao.
‘’ Chuo pia kina vituo vya ubunifu ambavyo vimekuwa vikifanya tafiti na kuwaibua vijana wanaofanya kazi kubwa za kutambuliwa’’,
hhlughakuwa uiJWT ulio mjUjumbe wa maofisa wa jeshi Tanzania umekutana na wanataaluma wa Chuo kikuu cha Taifa cha zanzibar kujadili namna ya kuratibu tafiti zinazoendeshwa katika taasisi zao.
Mkutano huo ulifanyika tarehe 18/12/2025 katika Makao Makuu ya SUZA tunguu Mkoa wa Kusini Unguja ulijadili kwa kina masuala muhimu yatakayowawezesha wanajeshi wanaotaka kuandika andika la kuanzishwa kitui cha Taifi cha Jeshi la wananchi wa Tanzania.
Akizungumza katika kikao hicho, Kanal Morris Ndeshiuta alisema azma ya kuanzishwa kwa kituo cha tafiti inalenga kuongeza uwekezaji na nguvu ya kijeshi hasa wakati huu ambao taasisi hiyo inatumia teknolojia yakisasa.
Alisema Jeshi la Polisi limefanya mambo mengine ambayo yanahitaji kutunzwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya vizazi vijavyo viweze kuyatambua.
‘’Tunashukuru sana kwa mchango wenu kwani tumepokea mawazo mengi na mazuri zaidi ya tulivyotarajia.’’, alisema Kanali Ndeshiuta aliyeongoza ujumbe watu saba kutoka JWTZ.
Aliongeza kuwa wameridishwa na michango na fursa walizopewa za kuwatumia wataalamu wa SUZA katika kufikia malengo waliyojiwekea.
Mkutano huo uliwashirikisha pia wakuu wa taasisi na wataalamu katika fani mbali mbali za zinazohusiana na masuala ya utafiti wa Chuo hiki ambao walichagia namna bora ya kuanzishwa kwa Kituo cha Tafiti cha Jeshi.