The State University Of Zanzibar

Chande aonya tafiti kufungiwa makabatini

Naibu Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Hamad Hassan Chande ameonya tafiti zinazofanywa na wahitimu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kufungiwa makabatini.
Hayo aliyasema wakati akifungua kilele cha Wiki ya Juma la Convocation kilichofanyika katika ukumbi ya Taasisi ya Utalii, kampasi ya Chuo Kikuu Maruhubi tarehe 22/12/2024.
Alisema iwapo utawekwa mkazo katika takufanya tafiuti na kuzifanyia kazi Zanzibar itasonga mbele sana kwani changamoto zinzaobainika zitaweza kutatuliwa.
‘’Tuongeze nguvu kwenye tafiti, tutasonga mbele zaidi ya tulipo iwapo tafiti nyingi ambazo tulizonazo hazitabaki katika makabati’’, alisisitiza.
Aliongeza kuwa viongozi wa SUZA wana fursa kubwa ya kuendeleza Chuo kwa kutanua wigo na kuingia katika mipaka yote ndani ya Tanzania.
‘’Tutanue wigo tuwekeze upande wa pili wa Tanzania bara kama vile Arusha, Tanga, Mtwara na kwengineko, ni mambo yanayowezekana, Tuandike ’’, alisisitiza.
Vilevile aliwataka wanafunzi kujitahidi kujiendeleza katika fani za elimu kwa kujiongezea maarifa kwenye ngazi mbali mbali ili kuiwezesha kauli mbiu ya SUZA ‘Suza Kichocheo cha Manadiliko’ kuendelea kuishi.
Katika mkutano huo, pia Mhe. Chande aliwatunuku zawadi na vyeti wanafunzi 47 waliofanya vyema katika masomo yao mbali mbali.
Katika mazungumzo hayo, alielezea uzoefu wake baada ya kumaliza masomo kwamba aliandika maadiko matatu ambayo yameleta manufaa na mabadiliko makubwa kwa jamii.
Alihimiza kuwa SUZA kinawaangalia wahitimu wake na kutarajia kuwa kila mmoja atakuwa na azma ya kuendeleza kuijenga SUZA kwa nguvu zote popote alipo.
Mhe. Alieleza kuwa alikotokea hakukuwa na maendeleo makubwa kinyume na wakati huu ambapo wanafunzi wa Kojani kisiwani Pemba wanasoma kwenye majengo ya kisasa yenye mafeni na viyoyozi.
‘’ Kipindi cha uongozi wa awamu ya nane ni cha kujivunia sana kwani kuna mabadiliko makubwa’’, alikumbusha Mhe Chande.