The State University Of Zanzibar

Kamati za ‘Convocation’ zatajwa

Mwenyekiti wa Kamati ya Mkusanyiko Kitaalamu (Convocation) Mhe. Riziki Juma Pembe amezindua rasmi Kamati za Mkusanyiko huo zilizowashirikisha wajumbe 14 ambapo mwengine anatarajiwa kutajwa hivi karibuni.
Akizungumza katika mkutano huo wa pili wa mwaka wa Mkusanyiko huo uliofanyika katika Kampasi ya Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA) ya Taasisi ya Utalii, Maruhubi tarehe 22/12/2024 alizitaja Kamati hizo kuwa ni pamoja na Kamati ya Kazi, Kamati ya Machapisho na Kamati ya Kutafuta Fedha.
Katika mkutano huo, Mhe. Riziki aliwakumbusha wajumbe kuhusu kuwajibika kwa dhati kwa ajili ya kuleta maendeleo kwani mkusanyiko huo unawahusu wanafunzi wote waliosoma katika Chuo Kikuu hicho.
Mapema katibu wa Kamati ya Convocation, Dk. Hashim Hamza Chande alisema Mkusanyiko huo ni muhimu kwa vyuo kuendelea kuwa karibu na vyuo vyengine mbali mbali na kuwatambua kuwa wao ni matunda ya kuleta maendeleo.
Alisema kuwa mkusanyiko huo unawakutanisha wanataaluma katika kipindi ambachoi nchi inaelekea kuashimisha miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anaadhimisha miaka minne tangu alipoingia madarakani mwaka 2020.
Katika mkutano huo, wajumbe walipewa fursa ya kutoa maazimio ambayo kwa mujibu wa Naibu Makamu Mkuu wa chuo. Dk. Hashim Hamza Chande kuwa yatawasilishwa katika Mkutano Mkuu wa tatu ujao.
Naye Dk. Ahmada Khatib alisema amefurahishwa na kasi ya utekelezaji majukumu yanayoikabili SUZA.
‘’Hakuna siku ambayi nimefarijika kama leo, Ile kasi ambayo tumeanzisha miaka 23 iliyoita inakwenda kwa kasi kubwa.’’,
Hali kadhalika, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo- SUZA, Bwana Ali Khamis alizungumzia mchango mkubwa wa wanawake katika nafasi za wanawake katika uongozi jambo ambalo halikuwahi kutokea katika kipindi cha miaka ya 1964 hadi 1972.
‘’ Wakati huo hakukuwa na Waziri, Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi mwanamke, sasa mpo wengi ila mnapaswa kupendana, muache fitna na majungu’’, alionya
Aidha, aliwataka wanawake kuungana mkono, na pale mwanamke anapogombania nafasi ya uongozi mwanamke mwengine analazimika kumpambania ili iwe rahisi kwake kushinda.