The State University Of Zanzibar

TANGAZO KWA WAOMBAJI WALIOCHAGULIWA AWAMU YA PILI MWAKA 2024/2025

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kinapenda kuutaarifu umma kuwa kimetoa orodha ya Majina ya waliochaguliwa kujiunga na masomo awamu ya pili kwa ngazi ya cheti, diploma na degree kwa mwaka wa masomo 2024/2025 kwa program mbali mbali kama zinavyojionesha hapo chini.

Chuo pia kinapenda kuwataarifu waombaji wote waliochaguliwa kuwa, wahakikishe wanaingia katika akaunti zao walizotumia wakati wa kuomba chuo kwa lengo la kupata barua za udahili (admission letter) pamoja na mambo mengine muhimu ya kujiunga na chuo.

kwa waombaji wa shahada ya kwanza (degree) ambao wamechaguliwa chuo zaidi ya kimoja (multiple selection), wanashauriwa kuingia katika akaunti zao na kuthibitisha (confirmation) kwa kutumia nambari ya siri (confirmation code) ambayo wamerushiwa na TCU kupitia nambari zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wakuomba chuo. Kama bado hujatumiwa nambari ya siri, ingia kwenye akaunti na uiombe kupitia sehemu iliyoandikwa request confirmation code. Tarehe ya wisho ya kufanya uthibitisho huo (confirmation) ni tarehe 21 oktoba 2024.

Aidha chuo kinawataarifu wale wote ambao hawakufanikiwa kuchaguliwa kwa awamu ya kwanza, wanaweza kuomba kozi nyengine ambazo wana sifa nazo na zilizotangazwa na chuo kwa awamu ya TATU itakayoanza tarehe 05/10/2024 hadi 09/10/2024. Kozi zinazotolewa awamu ya pili zimeambatanishwa katika tangazo hili.

Mwisho kabisa, Chuo kinawaomba waombaji wote wasisite kuwasiliana na maafisa udahili katika kampasi tafauti za chuo kwa msaada zaidi.