The State University Of Zanzibar

Suza yatoa elimu ya kilimo vijijini

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kupitia wanafunzi wake wanawapatia elimu ya Kilimo wanavijiji wanaowazunguka kwa lengo la kuimarisha sekta hiyo na kukabiliana na changamoto zinazowakabili.

Hayo yalisemwa na Bwana Ali Moh’d Ali ambaye ni mkufunzi wa Skuli ya Kilimo SUZA akiwa katika viwanja vya Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Kizimbani, Dole Mkoa wa Magharibi ‘A’ .

Wanafunzi wanaokamilisha masomo yao hufanya mazoezi ya vitendo katika vijiji vya karibu lakini baadhi ya wakulima huwafuata wataalamu hapo Kizimbani kwa ajili ya kupatiwa elimu ya kilimo na ufugaji.
‘’Tufanye kazi kwa pamoja ili tuone nguvu ya pamoja itakapotufikisha sisi tunaamini miaka michache ijayo SUZA itakuwa imeongeza wataalamu wengi katika fani ya kilimo na ufugaji’’, alisema Mtaalamu huyo.

Aidha, alifahamisha katika maonesho huu SUZA inawafundisha wananchi namna ya kutengeneza mizinga ya nyuki kwani mahitaji ya asali yamekuwa kwa kasi, program ambayo inafundishwa katika mtaala wa masomo ya Skuli ya Kilimo Kizimbani.

Katika maonesho hayo ambayo yamebeba kauli mbiu ‘KILIMO NI UTAJIRI TUNZA AMANI, TULIME KIBUNIFU’ yame inaonesha umuhimu wa kutunza miti ya asili yad awa nay a mboga kwa lengo la kuwapa hamasa wananchi na wao kuitunza.

Naye Bi Maryam Ali Hassan kutoka Skuli ya Kizimbani alifahamisha kuwa baadhi ya wananchi wanawasaidia kuwapatia baadhi ya miti yad awa za asili na mboga na wao wanaihifadhi baada ya kufahamishwa umuhimu wa miti hiyo.

Maonesho hayo yaliyoanza tarehe mosi mwezi Agosti yataendelea hadi tarehe 18.