The State University Of Zanzibar

Maonesho ya vijana yazinduliwa SUZA

Mke wa Rais wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Maryam Mwinyi leo amezindua maonesho ya Vijana ya Biashara na Uwekezaji katika viwanja vya makao makuu ya Chuo Kikuu cha Taifa cha SUZA, Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.


Maonesho hayo yalifanyika tarehe 10/08/2025 huandaliwa mahususi kwa ajili ya kuwajengea uwezo vijana walioko wasiokuweko skuli, vijana kwa jumla na wananchi wengine kuonesha, kutangaza na kuuza bidhaa wanazozizalisha.

Mama Maryam ambaye pia ni Mwanzilishi wa Taasisi ya Maisha Bora Foundation, amewahutubia wafanyabiashara na wananchi na waliofika kwenye maonesho hayo.


Akitoa maelezo kuhusiana na kazi zinazofanywa na SUZA, Makamu Mkuu wa Chuo hiki, Prof. Moh’d Makame Haji, alisema SUZA kinawalea vijana kuwa wabunifu na wanaweza kutengeneza bidhaa kwa kutumia rasiliamali zilizopo na wengine wamefanikiwa si kujiajiri tu lakini pia kufungua kampuni zao binafsi.

Wahitimu na wanafunzi wanaoendelea na masomo yao wana uwezo wa kutengeneza bidhaa za vyakula, dawa na urembo. Maonesho hayo ya siku yaliyoanza tarehe 9/08/2025 yanatarajiwa kufungwa 11/08/2025.