The State University Of Zanzibar

SUZA na Chuo Kikuu cha Osaka wakaribia kusaini mkataba wa kihistoria wamashirikiano

MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Prof. Moh’d Makame Haji amesisitiza kuwepo ushirikiano baina ya SUZA na Chuo Kikuu cha Amali cha Jiangsu cha China utakaoimarisha jitihada za serikali ya awamu ya nane chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi.

Aliyasema haya wakati akizungumza na ujumbe wa Chuo hicho ulimpomtemnbea katika ofisi za Makao makuu ya SUZA yaliyoko Mkoa wa Kusini Unguja hivi karibuni.

Alisema Serijkali ya Awamu ya Nane imeimarisha hospitali zake zote za Wilaya ambapo ni jukumu la SUZA kuzipatia watendaji wenye ujuzi unaotakiwa.

‘’Tunahitaji kuimarisha huduma zetu katika sekta ya afya, Taasisi ya elimu kama yetu inahitaji kuwapatia ujuzi katika utoaji wa huduma bora’’, alisisitiza Prof. Haji.

Alifahamisha kuwa SUZA kinahitaji ushirikiano na Jimbo la Jiangsu kufanikisha na kufikia malengo yaliyowekwa.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Amali cha Jiangsu, Bibi Cai Yimei alipokea kwa furaha wazo hilo na kueleza kuwa ushirikiano huo utajumuisha pia kuungana na Skuli zinazotoa taaluma katika masuala ya afya.

‘Tutakuwa na ushirikiano kwenye masuala ya afya na Skuli nyengine ili kuleta matumaini mapya kwenye utoaji wa huduma za afya Zanzibar’’, alifahamisha.