The State University Of Zanzibar

Hafla ya Utiaji saini Hati ya Mashirikiano baina ya SUZA na CGCLA

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar na Wakala wa Maabara na Mkemia Mkuu wamesaini Hati ya Mashirikiano ikiwa na lengo la kuimarisha mashirikiano ya Kitaaluma, Kitafiti hususan katika maeneo ya sayansi, maabara, ubadilishanaji wa maarifa, utaalamu na kiutendaji baina ya taasisi hizo mbili.

Akizungumza wakati wa utiaji sani huo Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Prof. Mohd Makame Haji amesema kuwa, makubaliano haya yanatarajiwa kufungua fursa mpya kwa wanafunzi na wataalamu wa SUZA kushirikiana moja kwa moja na CGCLA katika tafiti na kazi za kimaabara, pamoja na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta ya afya, mazingira na sheria kupitia ushahidi wa kisayansi.

Kwa upande wake Wakala wa Maabara na Mkemia Mkuu wa Serikali (CGCLA) Dkt Farid Mzee amesema kuwa mashirikiano haya yatasaidia kutimiza malengo ya Serikali ya utoaji huduma bora na ufanyaji wa tafiti zenye tija katika jamii.

Hafla ya utiaji saini ilifanyika katika ofisi za CGCLA zilizopo Maruhubi, Zanzibar tarehe 29 Mei, 2025. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Wakurugenzi kutoka CGCLA, wanasheria.

Ushirikiano huu unaashiria dhamira ya pamoja ya kuimarisha ubora wa huduma na elimu ya sayansi nchini.