The State University Of Zanzibar

Makamu Mkuu wa SUZA Ashiriki Mkutano Mkuu wa UNSATA

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Prof. Mohd Makame Haji, ameshiriki kama Mgeni Mualikwa katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wanafunzi Wauguzi Tanzania (UNSATA) uliofanyika leo tarehe 10 Mei 2025, katika Ukumbi wa Dkt. Shein, Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja.

Mkutano huo umejumuisha wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Uuguzi kutoka Vyuo mbalimbali nchini, ukiwa na dhamira ya kuimarisha taaluma ya uuguzi kwa misingi ya ushahidi wa kisayansi, kuhamasisha tafiti na kushirikiana kitaaluma ndani na nje ya Tanzania.

Mgeni Rasmi wa mkutano huo alikuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi), Mhe. Hamza Hassan Juma amewakilishwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Kukabiliana na Maafa ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Ndg. Makame Khamis Makame.