


Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimedhamiria kuanzisha mashirikiano na Chuo Kikuu cha Osaka nchini Japan yenye lengo la kukuza mashusiano kwenye Taaluma, Tafiti na kubadilishana wataalamu na wanafunzi kwenye maeneo ya lugha, utamaduni na afya. Haya yamesemwa na Makamu Mkuu wa SUZA Prof. Moh’d Makame Haji alipofanya mazungumzo na Mwakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Osaka Prof. Kumiko Miyazaki.
Naye Prof. Kumiko kwa upande wake amefurahi kukutana na uongozi wa Chuo na wapo tayari kwa ajili ya mashirikiano. Aidha amesema kuwa mashirikiano hayo yatasaidia kuleta wanafunzi wao Zanzibar kwa ajili ya tafiti mbalimbali wanazofanya. Kwa upande wa Makamu Mkuu wa SUZA ameahidi kuwa SUZA itasaidia kusimamia utaratibu wa upatikanaji wa vibali vya utafiti kwa wanafunzi na wanataaluma watakaotoka Osaka kuja Zanzibar kufanya tafiti zao.
Mazungumzo haya yalishirikisha Mkuu wa Idara ya Kiswahili kwa Wageni Bi. Shani, Mkuu wa Kituo cha Ukuzaji wa Taaluma za Kiswahili Ulimwenguni Bi. Fatma Soud Nassor na Mkuu wa Idara ya Sheria SUZA Dkt. Mtaib Abdulla Othman. Mazungumzo haya yamefanyika leo tarehe 7/05/2025 Ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo, Kampasi ya Tunguu