The State University Of Zanzibar

SUZA Yasaini Makubaliano Ya Ushirikiano Na Chuo Kikuu Cha Guru Kashi Kutoka India

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano wa kitaaluma na Chuo Kikuu cha Guru Kashi kutoka nchini India, ikiwa ni hatua muhimu katika kuimarisha ubora wa elimu ya juu na kupanua fursa za kitaaluma kimataifa.
Lengo kuu la ushirikiano huo ni kuanzisha kozi ya pamoja ya Shahada ya Uzamili katika Ujasiriamali (Master of Entrepreneurship) katika Skuli ya Biashara ya Chwaka ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar.
Kupitia makubaliano hayo, vyuo vyote viwili vitashirikiana katika kubadilishana wanataaluma, kuboresha mitaala ya masomo, pamoja na kuendeleza tafiti na ubunifu utakaowawezesha wanafunzi kupata ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira na kujiajiri.
Ushirikiano huu unatarajiwa kuongeza ubora wa ufundishaji na ujifunzaji, sambamba na kuwajengea wanafunzi uwezo wa ubunifu na ujasiriamali katika mazingira ya kimataifa.
SUZA inaendelea kujikita katika kupanua ushirikiano wa kimataifa ili kukuza elimu bora, utafiti na maendeleo endelevu.

Leave a Reply