


Mratibu Mkuu wa Mradi wa Mageuzi ya Elimu ya Juu Kiuchumi (HEET) Dkt. Kennedy Hosea, amewahimiza wakandarasi wa ujenzi wa mradi huo kuongeza kasi ya ujenzi ili kukamilisha kazi yao kwa wakati uliopangwa.
Alisema Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kiko karibu na wakandarasi kushirikiana nao kwa kila hali ili kutatua changamoto zinazotokea kama vile upatikanaji wa rasilimali na nguvu kazi.
Aidha, aliwaeleza wakandarasi hao kutumia rasilimali zilizopo katika eneo lao ili kuepusha mradi huo kusimama.
Naye Msaidizi Mratibu wa mradi huo kutoka SUZA, Dkt. Haji Ali Haji alisema kukamilika kwa mradi huo kwa wakati uliopangwa kutaijengea sifa SUZA na kuaminiwa kupewa miradi mengine mikubwa kutekelezwa.
Nae Kiongozi kiongozi wa mradi huo anaye shughulikia miondombinu na kazi za kiraia, Mhandisi Havington Kagiraki, ameelekeza kufanyiwa kazi kwa maelekezo yanayotolewa na wataalamu na Serikali ili kuepusha usumbufu wa upatikanaji wa majengo hayo.
Mhandisi mkaazi wa mradi huo, Mhandisi Aliki Nziku alisema vifaa vyote vilivyoagizwa na mkandarasi vinatarajiwa kufika mwezi Febuari mwaka huu jambo litakalowezesha kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.
https://www.instagram.com/p/DTSicrHCOL5/?igsh=OWM3MDRkbzNudWhr