Mhe. Mussa Azzan Zungu, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa UAE nchini Tanzania, Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Abdulrahman Almarzouqi pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda akiambatana na Ujumbe kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), katika kikao kilichofanyika tarehe 9 Januari, 2026 katika ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho, viongozi hao wamejadili kuhusu ushirikiano baina ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu hususan eneo la Akili mnemba (AI) katika kuongeza ufanisi wa shughuli za Bunge na kwenye maendeleo ya elimu nchini.
