





NAIBU Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha taifa cha Zanzibar (SUZA) anayeshughulikia masuala ya Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Salum Seif Salum amesema ushirikiano na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) utachangia kuitangaza SUZA kitaaluma kimataifa.
Hayo aliyasema katika mazungumzo yake kati ya ujumbe kutoka TCRA ambao unatoa mafunzo ya mawasiliano ya kimataifa (International Telecommunication Union- ITU) uliofika Chuoni hapo kwa ajili ya kujitambulisha na kuitaka kuwa mwanachama wa mpango huo.
Uanachama huo utaiwezesha SUZA kufaidika na fursa za masomo kwa wanafunzi na watendaji wake wengine, kuitangaza SUZA kimataifa, kushiriki kwenye mijadala mbali mbali ya kitaaluma inayohusiana na teknolojia, na uvumbuzi.
Naye, Mhandisi kutoka TCRA Bi. Sophia Nahoza mafunzo hayo yanalenga ya kuwawezesha vijana kwenye taasisi za kielimu kufanya kazi zao kwa njia za kisasa na kupata matokeo ya haraka.
Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi za makao makuu ya SUZA zilizopo Tunguu mkoa wa Kusini Unguja tarehe 17/12/2025 ambapo yameanza maandalizi ya kukiwezesha Chuo kujisajili iili kuwa mwanachama halali atakayefaidika na fursa zilizopo.