The State University Of Zanzibar

Wema wakagua miradi ya ujenzi Tunguu

Ujumbe wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar (WEMA) ukiwa pamoja na watendaji na maofisa wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ukiongozwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Khadija Salum Ali ukikagua miradi ya maendeleo inayotarajiwa kuwekwa jiwe la msingi katika kipindi cha shamrashamra za Mapinduzi ya Zanzibar mwezi Januari mwakani.

Katika ziara hiyo, walikagua majengo mawili ya maabara ambalo limefikia asilimia 54 na jengo la Kilimo ambalo limefikia asilimia 59 wa ujenzi. Kwa ujumla, ujenzi huo umefikia asilimia 55.
Mkandarasi wa majengo hayo, Mohammed Builders ameshauriwa kuongeza nguvu kazi ili kukamilisha ujenzi huo kwa wakati uliopangwa. Ukaguzi huo ulifanyika kwenye maeneo ya ujenzi katika kampasi ya Chuo Kikuu cha taifa cha Zanzibar tarehe 17/12/2025