








Wakaguzi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Tanzania wameridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi (HEET) wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).
Hayo yalisemwa na wakaguzi hao wakati wakiwa katika kikao na Watendaji (PIU) wa Mradi huo kwa lengo la kukagua mendeleo ya mradi pamoja na kusikiliza changamoto zinazoukabidili mradi huo.
Aidha, wamesema mradi unaendela vizuri kwani umefikia asilimia 49 hadi leo tarehe 02/09/2025 kwa tathmini ya majengo yote yaani jengo la Maabara na Jengo la Skuli ya Kilimo.
Kikao hicho kilihusisha pia timu ya Mkandarasi ambaye ni Mohammedi Builder na Mshauri Elekezi ambaye ARQES katika Ofisi za ujenzi Tunguu Zanzibar. @wizara_elimutanzania