The State University Of Zanzibar

SUZA imefikia asilimia 39 ya utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi (HEET)

Chuo Kikuu Cha Taifa Zanzibar (SUZA) kimefikia asilimia 39 ya utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi (HEET) katika ujenzi wa majengo ya Maabara na Skuli ya Kilimo, kutokana na tathmini hiyo Mkandarasi yupo ndani ya muda.