The State University Of Zanzibar

MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YAFIKIA KIKOMO, SUZA YAONESHA MCHANGO WAKE KATIKA MAENDELEO YA ELIMU

Leo tarehe 13 Julai 2025, Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yamefikia tamati katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa, Dar es Salaam. Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kilikuwa miongoni mwa taasisi zilizoshiriki kikamilifu katika maonesho hayo ya siku kumi na nne, yakilenga kuonesha bidhaa, huduma na teknolojia mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Katika kushiriki kwake, SUZA kama mdau muhimu wa maendeleo katika sekta ya elimu, ilitumia fursa hii kuonesha namna elimu ya juu inavyoweza kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi kwa vijana. Kupitia banda lao, SUZA iliwaelimisha wananchi juu ya fursa mbalimbali za masomo zinazopatikana chuoni hapo pamoja na namna ambavyo wanafunzi wanaweza kujikwamua kiuchumi kupitia taaluma wanazosomea