


Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Dk. Hashim Hamza Chande SUZA imetoa shukurani kwa kupata heshima kuchaguliwa kuwa ni mahala pa kutolewa mhadhara wa masuala ya anga.
Hayo aliyasema wakati akimkaribisha mtaalamu ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Omani Space Astronomical Society, Bw. Abdulwahab Suleiman AlBusaid aliyefika nchini kwa ajili ya kutoa taaluma ya anga na telescope kwa wanataaluma na wanafunzi na walimu wa SUZA na maofisa wengine mbali mbali kutoka taasisi nyenegine zinazoshughulikia masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa ambao wamealikwa kushiriki.
‘’ Mjadala huu utaongeza kasi ya uhusiano baina ya taasisi hiyo na SUZA kwa kuwaunganisha na wataalamu wa anga’, alisema Dk. Hashim.
Naye Bw. Albusaid alisema kuwa amewahi kuzungumza na watu wengi lakini hakuwahi kusikia kuwa wanataaluma kuhusiana na Biolojia, Kemia, Hisabati, Sayansi, hali ya hewa na mengine yanayohusiana nayo, hivyo SUZA imempa faraja kubwa kuiunganisha kuendelea na kupata taaluma za astronomy na astrophysic.
Alisema ametembelea Website ya SUZA na ameridhishwa na maudhui aliyoyaona kwa kumuwezesha kujifunza mambo mengi.
Mtaalamu huyo ana uzoefu mkubwa katika masuala ya anga, anaishi nchini Oman ambaye ameondoka Afrika ya mashariki zaidi ya miaka 40 iliyopita.
Mafunzo hayo yamewashirikisha walimu wa SUZA wa masomo ya Fizikia, Jiografia, Kemia, Historia, mabadiliko ya tabia nchi, na taasisi nyengine kama vile Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.