


Makamu Mkuu wa Wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Prof. Moh’d Makame Haji, ameelezea kuridhishwa na Shirika la Maendeleo la NORAD la Norway linavyoendelea kuiunga mkono SUZA katika utekelezaji wa mairadi mbali mbali ya kitaaluma.
Katika mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya SUZA Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja akiwa na Mratibu wa Miradi ya NORAD Afrika, Grete Benjaminsen, Prof. Haji alisema ushirikiano wao Shirika hilo umeleta mabadiliko kwa kuwapatia fursa wafanyakazi na wanafunzi kujiunga na programu mbalimbali.
‘’Tunapata kuwezeshwa, wapo wanafanyakazi wengi wanafanya program kadhaa za Uzamivu na Uzamili, tuna furaha sana juu ya maendeleo haya’’, alisema Prof. Haji. Naye, Bibi Grete alieleza kuwa Shirika lake linadhamini masuala ya kitaaluma katika nchi za Afrika na taasisi za utafiti na pia wanatafuta wadau watakaowaunganisha na SUZA ili kuijengea uwezo zaidi.