The State University Of Zanzibar

Ushirikiano SUZA, ubalozi wa Marekani waimarika

Naibu Makamu Mkuuwa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Dkt. Hashim Hamza Chande, amekutanana Bw. Chad Morris, ofisa wa masuala ya umma na  Karen Nasso, ofisa wa “American Spaces,”  kutoka Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania.

Mkutano huo uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya Chuo Tunguu tarehe 15/04/2025  ulilenga kuimarisha ushirikiano na kati ya SUZA na Ubalozi huo ambapo  Bw. Morris alitumia fursa hiyo  kuaga kufuatia kukamilisha muda wake wa kazi hapa Zanzibar.

 Katika mazungumzo hayo, Bw. Morris alihamasisha SUZA kueleza mahitaji ambayo Chuo kingependa kupata msukumo, hasa katika kukuza uwezo wa lugha ya Kiingereza kwa walimu na wanafunzi. Pia alieleza kuw kuwa masomo mengine yanayohitaji kupewa kufundishwa  kwa Kingereza  yanapewa kupewa kipaumbele.

Naye, Mkuu wa Skuli ya Elimu, Dkt. Said Khamis, alielezea utayari wa SUZA kupokea mtaalamu wa kufundisha lugha ya Kiingereza, ambaye anatarajiwa kuanza kazi mwezi Oktoba mwaka huu.

Hali kadhalika alisisitiza umuhimu wa kupatiwa mafunzo  kuhusu maandiko ya kitaaluma, utafiti na kuaznisha darasa maalum la  kufundisha lugha ya Kingereza na masuala ya akili mnemba (AI). 

Mkutano huo ulijumuisha pia viongozi wa Skuli nyengine za SUZA, wakiwemo Dk. Ali Adnan (Mkuu wa Skuli ya Kompyuta na Mawasiliano), Dkt. Abdallah Mkumbukwa (Mkuu wa Skuli ya Sayansi Asili na Sayansi Jamii), na Dkt. Said Juma (Mkuu wa Skuli ya Elimu).

 Ushirikiano huo ulionekana kuwa na fursa nyingiza kuboresha sekta ya elimu kupitia mchango wa ubalozi wa Marekani.