


MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Prof. Moh’d Makame Haji amewakumbusha wadau wa Chuo hiki kuzingatia kuweka kipengele cha kulinda maadili na kutunza nidhamu kwenye Sera ya Michezo ya SUZA.
Alisema washiriki wa michezo watambue kuwa wao ni wanafunzi wa SUZA wakati wakiendelea na michezo walinde heshima zao, Chuo na nchi kwa jumla.
Alikumbusha kuwa suala la maadili ni vyema likaonekana kwa uwazi katika sera hasa ikizingatiwa kuwa linahusisha muingiliano mkubwa baina ya wanafunzi na hata walimu ama wa ndani au wa vyuo vyengine vya nje.
Akizungumza katika mjadala wa Sera ya Michezo uliofanyika makao makuu ya SUZA Tunguu mkoa wa Kusini Unguja tarehe (21/03/2025), Prof Haji alisema wakishiriki michezo yao wafahamu kuwa ni wanafunzi wa SUZA na watapaswa kusimamia misingi ya kinidhamu na kuendelea michezo katika kulinda maadili .
Alifahamisha kuwa michezo inakwenda sambamba na azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuimarisha hamu ya vijana kushiriki, kuchangia maendeleo ya nchi na hasa kupata ajira hivyo kuna haja ya kuweka mfumo bora wa uendeshaji wa shughuli hizo.
‘’ Sera inafaa kuwa na kipimo kizuri cha kuwazingatia wanafunzi wanaoshiriki michezo endapo ratiba za masomo zitaingiliana na muda wa masomo’’, alisisitiza.
Alifafanua kuwa michezo ni jambo huru ambalo halimbani mshiriki katika masuala ya kiimani wala kitamaduni ila kwenda kinyume na maadili ni jambo ambalo haliwezi kuvumilika.
‘’Tunataka watendaji na wanafunzi ambao wanahitaji kupata muda kuimarisha afya baina yao na taasisi nyengine kupitia michezo, kujenga uhusiano na ustawi bora ndani na nje ya Chuo’’, alisema Prof. Haji.
‘’ Hii ni sekta muhimu katika sekta ya m kitaifa zinazoangaliwa kuongeza ajira ( fursa), kuburudisha kufurahi kukusanyika na kutoka nafasi ya kushiriki katika matukio mbali mbali
Aliongeza kuwa michezo ni sekta rasmi inayochangia maendeleo ya nchi, kuitambulisha kwa kujenga ushirikiano mwema na kuiwezesha kujitangaza katika mambo mabli mbali.
Naye, Mratibu wa Michezo wa SUZA wa ofisi ya Ustawi, Ndg. Hassan Khairalla, alisema SUZa ilikosa muongozo kwa muda mrefu na hivyo kuamua kutengeneza sera ili Chuo kiendeshe mambo yake kwa utarabu wa kisheria.
Naye, Mwakilishi wa Kampuni ya Halotel, Daud Daud, ambaye ni mdau wa kwanza kujitokeza kushirikiana na SUZA katika sekta ya michezo alithibitisha kuiendeleza sekta na hiyo kwa ushirikiano mkubwa.
Mapema Rais wa Serikali ya Wanafunzi ya SUZA, Bi Mwanamkuu Jega Bakari ameushukuruuongozi wa wa SUZA kwa kuwa karibu na Serikali ya wanafunzi jambo linachangia kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Mkutano wa kujadili Sera ya Michezo ya SUZA huu wa wa wadau uliowashirikisha wanafunzi kutoka kampasi zote za chuo kikuu, wakuu wa taasisi za SUZA na wageni wengine walioalikwa kuchangia sera hiyo.