Waziri wa Waziri wa Nchi (OR) Katiba, Sheria na Utumishi wa na Utawala Bora, Mwalim Haroun Ali Suleiman, ametoa wito kwa Taasisi za Elimu za Zanzibar kufanya tafiti nyingi zenye matokeo yatakayoleta mabadiliko kwa maendeleo ya jamii.
Akifungua Kongamano la Kitaaluma la kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Malipo Zanzibar lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi leo (21/09/2024), Mwalim Haroun alisema kuwa licha ya umuhimu wa kutekeleza taasisi hizi zinahitaji kuungwa kwa kupatiwa bajeti maalum. Aidha, aliongeza jitihada za kuimarisha elimu zimekuwa zikichukuliwa na uongozi awamu zote nane tangu mwaka 1964 hadi leo kuwa tunapaswa kutambua juhudi za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
‘’Tumpongeze Dk. Hussein Ali Mwinyi ametuokoa sana’’, alikumbusha.
Aidha, aliongeza kuwa awamu ya nane ya uongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imefanya mageuzi mkubwa ya elimu hasa kwa upande wa kupatikana vifaa vya kisasa, kuongeza bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Elimu na miundombinu mingine.
Katika hatua nyengine, Mwalimu Haroun Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi alifahamisha kuwa Mzee Karume alifanya jiithada kubwa ya kupambana ubaguzi wa matabaka baina ya watu wenye uwezo ambao walipata fursa zote za elimu na ajira na wasiokuwa na uwezo na wanaotoka mashamba.
Akielezea uzoefu wake katika maisha kabla na baada ya Mapinduzi alisema kuwa yeye binafsi ni mwathirika wa ubaguzi huo katika familia wakati huo.
Mapema, Prof; Moh’d Makame Haji Alifahamisha kuwa Kongamano hili linaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 60 ya mapinduzi ambayo ndiyo yaliyoleta mageuzi makubwa ya elimu.
Alifahamisha kuwa wananchi walikosa fursa ya elimu katika ngazi mbali mbali kutokana utawala wa wakati huo, suluhisho lililoletwa na muasisi wa Taifa hili, Hayati Abeid Amani A Karume, hali inayoendelea kuimarika katika awamu nane mfululizo za uongozi wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar.
‘’SUZA ni miongoni mwa matunda ya Elimu bila Malipo kufuatia kupitishwa kwa sheria mwaka 1999 na Chuo kuanza rasmi mwaka 2021 kikiwa na Idara mbili (2) za taaluma na wanafunzi 108 ambapo kwa sasa kina skuli tisa (9) na taasisi mbili na sasa kuna wanafunzi 7045 na programu zaidi ya 60 ’, alisema.
Aidha, aliongeza kuwa SUZA imekuwa mhimili mkubwa wa kufanya tafiti, kutoa taaluma na kutoa ushauri elekezi Serikalini, kutoa suluhisho kwa jamii kjuu ya changamoto mbali mbali zinazowakabili.
Aliongeza kuwa tangu SUZA ilipoanzishwa imezalisha mwahitimu zaidi ya 18,000 uzamili na uzamivu, watu wa aina hii ni vigumu kufanya kazi na degree na watu wa aina hii kufanyakazi katika kwa hivyo eneo la msingi linaloangaliwa ni kuzalisha vijana wenye ustadi wa ufundi na ujasiriamali.
’’ SUZA imefanya mazungumzo na taasisi mbalimbali ambazo ziko tayari kuwapokea wahitimu wetu watakaoweza kufanya kazi nao’, alisema Prof. Haji. Akimkaribisha mgeni rasmi, Waziriwa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe. Lela Mohammed Mussa, aliwakumbusha wanakongamano na wananchi kwa jumla kuyaenzi Mapinduzi kwani kwani yamewakomboa wanyonge.
Alieleza kuwa jamii inapaswa kutambua kuwa elimu ni chachu ya mabadiliko na maendeleo ya nchi.
Naye Mhe. Balozi Mohammed Hamza ambaye ni Mwenyekiti wa Kongamano hilo, aliwahimiza wananchi wa Zanzibar kuenzi na kutunza tunu ya Elimu Bila Malipo kwani ndiyo iliyowakomboa wananchi wanyonge wa visiwa vya Unguja na Pemba.
Akifunga Kongamano hilo, alisisitiza kuwa elimu inayotolewa itosheleze mahitaji ya sasa na yajayo sambamba na kupitiwa sera, mipango, mikakati na uongozi wa Wizara ya Elimu kwani mabadiliko ya dunia yanakwenda kwa haraka mno.
Muwasilishaji mada , Dk. Bakari Ali Silima kutoka Chuo cha Mafunzo ya Amali Zanzibar alisema maendeleo kwenye fani ya mafunzo ya amali yamekua kutoka fani nne lakini hivi sasa kuna fani 22 zinazofundishwa Unguja na Pemba, huku kukiwa na vyuo 57 vikiwemo 16 ya Serikali na 41 ni vya taasisi za binafsi.
Wataalamu wengine waliowasilisha mada ni pamoja na Mhe. Balozi Amina Saluma Ali Elimu, Uchumi na Fedha, Dk. Cosmas Mnyanyi Elimu Mjumuisho, Bw. Abdullah Mzee Abdullah Elimu Bila Malipo na Bw. Amour Mtumwa Ali Elimu na Fursa za Utalii.
Kongamano hilo lilloandaliwa na SUZA limewashirikisha watu mbalimbali wakiwemo wasomi, wanataaluma katika fani mbali mbali, wakurugenzi, wanafunzi kutoka Vyuo za Zanzibar na skuli mbalimbali za SUZA.