The State University Of Zanzibar

SUZA, UNDP kuendeleza ushirikiano

Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Prof. Moh’d Makame Haji amefanya mazungumzo na ujumbe kutoka Shirika la Maendeleo la UNDP kuhusiana kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya taasisi hizo.


Mazungumzo hayo ambayo pia yaliwashirikisha watendaji wa UNDP yalifanyika leo 23/09/2024 katika Ofisi za makao makuu SUZA Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja, ambapo kiongozi wa ujumbe huo ambaye pia ni Mwakilishi Mkaazi wa Shirika hilo, Bw. Shigeki Komatsubara alisema kuwa uchumi wa buluu unazidi kuwa mashuhuri sana katika ukuaji wa uchumi wa Zanzibar.


Aliongeza kuwa uchumi huo una fursa nyingi za kuwawezesha watu kufikiria namna gani wanaweza kuzalisha fedha na kuyataja miongoni mwa maeneo muhimu ya uchumi huo kuwa ni ukulima wa mwani, mabadiliko ya hali hewa, usafirishaji na utalii na masuala mengine ya kibiashara.


‘’Dira za viongozi ni muhimu sana’’, alisema akigusia sera ya uchumi wa buluu iliyoasisiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi ambayo SUZA inaandaa mazingira ya kuitekeleza


Watu hawana hofu na usalama wao, na wakianza kufikiria kuhusu jambo hilo hapo ndipo watakapoweza kufanya biashara na kuzalisha fedha nyingi.


Akitoa mfano wa nchini kwao Japan alisema wana uwezo wa kuwekeza katika nguvu kazi pekee kwa hivyo elimu inapewa umuhimu wa kwanza kabisa na hivyo kuishauri SUZA kuona kuwa Chuo ni kitega uchumi cha baadaye.


Aidha, alivutiwa na maelezo Mkuu wa Chuo SUZA Prof. Haji ya namna inavyokua tangu ilipoanza kutoa mafunzo kwa wazawa na wageni kutoka wanafunzi 83 kwa kuwa na Idara mbili hadi wanafunzi 7045 hivi sasa kwa kuwepo Idara tisa na taasisi mbili zinazotoa mafunzo na program kwa mujibu wa mahitaji yanayoendana na ulimwengu.


Kutokana na mazungumzo hayo, Bw. Komatsubara aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa SUZA katika kujengea uwezo kwa wanafunzi pamoja na wafanyakazi hasa katika maeneo ya mafunzo ya uwezo (competences) kwa kushirikiana na vyuo vyengine vya kimataifa na miundombinu ya TEHAMA.


Naye Prof. Haji alisema alizifafanua Idara na taasisi zinazotoa kozi na programu pamoja na kuyataja maeneo mengine wanayofanyia kazi ikiwa kama vile; utafiti, ushauri kwa serikali na kuzisaidi jamii kutambua changamoto wanazokabiliana na kuzitafutia suluhu.

Naye, Dkt. Abubakari Diwani, msimamizi wa moja ya moiradi iliyofadhiliwa na shirika hilo Mradi wa wasteX, alisema wana matarajio makubwa ya kutekeleza majukumu yao iwapo watawezeshwa katika miundombinu ili wanafunzi waweze kubuni fikra mpya sambamba na ukusanyaji wa takwimu.


‘’Tuna jukumu la kufanya kazi na Serikali na tunafanya kazi nayo katika masuala mbalimbali likiwemo la uchumi wa buluu.