The State University Of Zanzibar

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Taaluma, Skuli na taasisi mbalimbali ndani ya SUZA

Leo tarehe 15 Oktoba 2025, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi, Prof. Abdi Talib Abdallah, alitembelea Skuli na taasisi mbalimbali ndani ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar – SUZA kwa lengo la kuzitembelea kampasi za Chuo na kukutana na Wakuu wa Skuli pamoja na Wakuu wa Idara.


Ziara hiyo ilianza katika Taasisi ya Utalii Maruhubi, ambapo Prof. Abdi Talib Abdallah akisisitiza nafasi muhimu ya utalii katika kuchochea uchumi wa Zanzibar. “Utalii ni mnyororo mkubwa wa maendeleo ya Taifa letu, na hivyo utafiti wa kisayansi katika sekta hii ni muhimu sana,” alisema Prof. Abdi Talib Abdallah.

Baada ya hapo, alitembelea Skuli ya Kiswahili na Lugha za Kigeni, ambapo alikutana na Mkuu wa Skuli pamoja na Wakuu wa idara mbalimbali. Hapa, Prof. Abdi Talib Abdallah alibainisha umuhimu wa lugha za kitaifa na za kigeni katika kukuza utafiti unaoweza kuleta tija katika masuala ya kiuchumi na kijamii. Alihimiza kuimarisha utafiti wa lugha kama chombo cha kuelekea kwa soko la kimataifa.


Mwisho wa ziara kwa siku ya leo ni Skuli ya Kilimo Kizimbani, ambapo Prof. Abdi Talib Abdallah alikutana na wakuu wa Idara pamoja na Kaimu Mkuu wa Skuli ambapo alisisitiza umuhimu wa kufanya Utafiti kwa kusema “Utafiti ni moja ya silaha zetu kuu za kupambana na umaskini na kuleta maendeleo endelevu ya taifa,”