Chuo Kikuu cha Bonga kilichopo nchini Adis Ababa, Ethiopia kimekiomba Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kushirikiana nao kuikuza taaluma hususan kuieneza lugha ya Kiswahili nchini humo.
Katika mazungumzo hao yaliyoushirikisha uongozi wa Chuo yaliyoongozwa na Mkurugenzi wa Shahada za Awali, Dk. Khamis Haji Salum , Rais wa Chuo cha Bonga Dk. Petros WOldegiorgis alisema lugha ya Kiswahili imekuwa na wazungumzaji wengi ambapo Chuo chake angependa kuwa sehemu ya kuimarisha lugha hiyo.
‘’Chuo ninachokiongoza kinafundisha lugha ya Kirusi sasa nataka kifundishe na lugha ya Kiswahili ambacho ndio utambulisho wa lugha za Afrika’’, alisema Rais WOldegiorgis.
Aidha, aliongeza kuwa ana furaha kubwa sana kuona kuwa SUZA ni kituo kinachofundisha lugha ya Kiswahili jambo ambalo litasaidia kukuza ushirikiano wa kitaaluma sambamba na kubadilishana wataalamu wafanyakazi na wanafunzi, kufanya tafiti na kuimarisha utamaduni wa kiafrika.
Rais WOldegiorgis alisema ana dira ya kuwepo Umoja wa Vyuo Vikuu vya Afrika ambao utasaidia kuenzi falsafa za viongozi mashuhuri wa Kiafrika akiwemo Hayati Mwalimu Myerere na Kwame Nkuruma.
Alifahamisha kuwa Afrika ina kila historia, lugha, rasilimali utamaduni mambo ambayo yanapaswa kusimamiwa na vizazi vilivyopo kwa ambao wataunganishwa kupitia Umoja wao kuwa kuzingatia falsafa za viongozi waliopita na
Nae Mkurugenzi Haji alimueleza Dk. Alimueleza Dk. WOldegiorgis kuwa SUZA haina haina pingamizi na ushirikiano wa kitaaluma kwani ndio dira inayochangia kuleta mabadiliko makubwa ya kitaaluma kwa kufanya tafiti za pamojan kubadilishana wataalamu.