The State University Of Zanzibar

SUZA, Emirates watiliana saini ujenzi wa dakhalia

SUZA, Emirates watiliana saini ujenzi wa dakhalia Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimetiliana saini na mkandarasi Emirates Company Ltd katika ujenzi jengo la ghorofa n e la Dakhalia ya Wanafunzi Wanawake unaofadhiliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Tukio hili linaashiria hatua muhimu katika juhudi za kuimarisha fursa za elimu na kukuza mazingira bora ya kujifunzia kwa wanafunzi wote, hili ni miomgoni mwa utekelezaji wa vipaumbele v a Serikali ya Awamu ya Nane chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Jengo hili ambalo litasimamiwa na Kampuni ya Arqes Afrika litakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 wanawake kwa wakati. Ujenzi huo utakaoanza mara tu baada ya utiaji saini unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 15 na utagharimu shilingi bilioni 10.354. Dakhalia hiyo ya kisasa itakuwa na huduma zote za msingi na kuweza kufikika kila mahala hasa kwa watu wenye mahitaji maalum na itajengwa katika Kampasi ya Chuo Kikuu cha Taifa SUZA Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.

Upatikanaji wa makaazi bora na salama ni muhimu kwa mafanikio ya kitaaluma, ambapo mradi huu unalenga kutatua changamoto zinazowakabili wanafunzi wa Kike zinazoweza kuzuia kufikia malengo yao ya kupata elimu. Kila mwanafunzi ana nafasi ya kustawi katika safari yake ya kitaaluma.

Wazo la kujenga dakhalia lipo tokea mwaka 2012 tulipohamia katika kampasi ya Tunguu ambapo hatua mbalimbali zilichukuliwa ikiwemo kujumishwa kwenye maandiko ya miradi ya maendeleo.

SUZA inaipongeza Serikali ya Awamu ya Nane ya Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuwa na maono na nia thabiti va kutekeleza miradi ya maendeleo kwa manutaa yawananchi.

Tunapoanza mradi huu, tukumbuke kuwa hii ni sehemu ya maono ya muda mrefu ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar – maono ambayo yanasisitiza upatikanaji wa elimu kwa wote, bila kujali jinsia. Malengo ya Chuo ni kuandaa mazingira ambayo yanakuza vipaji, yanakuza uvumbuzi, na yenye kuandaa wanafunzi kuwa viongozi bora katika jamii zao na Taifa kwa ujuamla