The State University Of Zanzibar

Baraza la Chuo lakutana na wanataaluma

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Bi Hamida Mohammed Ahmed amesema utekelezaji majukumu ya Baraza umechangia kuweka mazingira mazuri ya utoaji wa huduma za Chuo.


Akizungumza katika mkutano wa pamoja na wanataaluma na wajumbe Kamati mbali mbai za SUZa uliofanyika makao makuu ya SUZA Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 28/01/202, alisema SUZA imekuwa na mabadiliko makubwa katika utoaji wa elimu na kuimarishwa miundombinu ya Chuo.


Aidha, aliwashukuru wajumbe wa Baraza la Chuo na wanataaluma kwa ushirikiano mkubwa wanaouonesha unaochangia kufanikisha malengo yaliyowekwa na kuahidi kuwa mkutano kama huu utakuwa wa kudumu kwa ajili ya kutatua changamoto zinazojitokeza.


Mapema Makamu Mkuu wa SUZA, Prof. Moh’d Makame Haji alifahamisha kuwa SUZA inashirikiana na wadau mbali mbali wakiwemo wataalamu kutoka Kamisheni ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), na vyuo vyenye sifa na uzoefu mkubwa katika utoajihuduma.


‘’Tunatengeneza mazingira rafiki yatakayokivusha Chuo hatua nyengine ya mafainikio, fahamike kuwa baadhi ya mambo yanayofanywa na SUZA ni lazima yapite Serikali kuu kabla ya kutekelezwa’’, alikumbusha.


Alisema pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana, suala la tafiti linahitaji kuwekewa mkazo mkubwa.


Naye Mwenyekiti Kamati ya Ustawi ya SUZA, Bi Salma Saadat, alipendekeza kuwa wanafunzi washajiishwe kuwasilisha changamoto zao katika Kamati za Ustawi za Chuo.


Rais wa Serikali ya Wanafunzi ya SUZA (SUZASO), Mwanamkuu Jega aliwashauri wanataaluma kutumia lugha za busara kwa wanafunzi wanapotoa maelekezo.


Alithibitisha kuwa wako tayari kuongozwa na wanataaluma kwani wao ni watu wa mwanzo wanaoshuhudia mwanzo maendeleo yao ya elimu.