WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Mhe. Sharif Ali Sharif ametoa wito kwa Taasisi za Elimu Zanzibar kuendeleza vipaji vya wanafunzi kuanzia maandalizi hadi sekondari.
Alisema hatua hiyo itachangia kuwawezesha kuwa mahiri na wabunifu katika fani mbalimbali kulingana na mazingira wanayotokea.
Akizungumza katika sherehe ya maadhimisho ya miaka 60 ya Elimu Bila Malipo iliyofanyika katika viwanja vya Mapinduzi Square Kisonge mkoa wa Mjini Unguja, alisema usimamizi wa karibu wa vipaji utawasaidia kutatua changamoto ya ukosefu ajira na kuitangaza Zanzibar kimataifa.
‘’Wanafanya mambo makubwa, wanatengeneza vitu vya mapambo, endeleeni kufanya bidii katika sanaa wanazojishughulisha nazo, zitawasaidia hapo baadaye’’, alisema Mhe. Sharif.
Mapema, Mkurugenzi Idara ya Michezo na Utamaduni, Bi Hafsa Aboud Talib alisema maonesho haya ya kitaaluma yamezishirikisha taasisi za elimu 20 zikiwemo za Serikali na za binafsi.
Miongoni mwa taasisi hizo ni; kama vile Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Elimu Zanzibar, Chuo cha Mafunzo ya Amali cha Zanzibar, Zanzibar School of Health (ZSH), Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu Zanzibar Madrassa Resource Center, Room to Read na Sazani.
‘’ Katika maonesho haya ya kitaaluma, tunalenga wazazi pia wake wajifunze ili wakiwa majumbani mwao waweze kuwasaidia watoto wao wakiwa wa majumbani’’, alisema Bi Hafsa.
Mtaala wa unaotumika hivi sasa unalenga kumuwezesha mwanafunzi kuwa na maarifa, ujuzi na mwelekeo kwa lengo la kumuandaa na kumjenga kuwa mtedaji kama vile kubuni vitu mbali mbali vya ujasiriamali.
Wizaraya Elimu na Mafunzo ya Elimu imefanya mageuzi makubwa ya Elimu katika mtaala ambapo inalenga kuwajenga wanafunzi kuwa na ujuzi na maarifa.
Hivi sasa watasoma elimu ya amali kwa kujishughulisha na kazi za ufundi, ushoinaji, uvuvi utengenezaji vifaa na fani nyengine kuanzia mwakani 2025.
Katika mpango huo skuli 33 ndizo zitakazoanza utekeleazaji huo kwa hatua ya kwanza ambapo kutakuwa na mafunzo