Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kinapenda kuutaarifu umma kuwa kimetoa orodha ya Majina ya waliochaguliwa kujiunga na masomo awamu ya kwanza kwa ngazi ya Cheti, Stashahada na Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2024/2025 kwa programu mbali mbali kama zinavyojionesha hapo chini.
Chuo pia kinapenda kuwataarifu waombaji wote waliochaguliwa kuwa, wahakikishe wanaingia katika akaunti zao walizotumia wakati wa kuomba Chuo kwa lengo la kupata barua za udahili (admission letter) pamoja na mambo mengine muhimu ya kujiunga na Chuo.
kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza (Degree) ambao wamechaguliwa Chuo zaidi ya kimoja (multiple selection), wanashauriwa kuingia katika akaunti zao na kuthibitisha (confirmation) kwa kutumia nambari ya siri (confirmation code) ambayo wamerushiwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kupitia nambari zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wakuomba Chuo. Kama bado hujatumiwa nambari ya siri, ingia kwenye akaunti na uiombe kupitia sehemu iliyoandikwa request confirmation code. Tarehe ya mwisho ya kufanya uthibitisho huo (confirmation) ni tarehe 21 septemba 2024.
Aidha Chuo kinawataarifu wale wote ambao hawakufanikiwa kuchaguliwa kwa awamu ya kwanza, wanaweza kuomba kozi nyengine ambazo wana sifa nazo na zilizotangazwa na Chuo kwa awamu ya PILI itakayoanza tarehe 03/09/2024 hadi 21/09/2024. Kozi zinazotolewa awamu ya pili zimeambatanishwa katika tangazo hili. Mwisho kabisa, Chuo kinawaomba waombaji wote wasisite kuwasiliana na maafisa udahili katika kampasi tafauti za chuo kwa msaada zaidi.
CERTIFICATE PROGRAMMES
# | COURSE | CODE |
---|---|---|
1 | Certificate in Hospitality Operation | CHO |
2 | Certificate in Journalism | CJ |
3 | Certificate in Librarianship and Information Studies | CLIS |
4 | Basic Technician Certificate in Tour Guiding | CTG |
5 | Basic Certificate in Computing and Technology | CCT |
6 | Certificate in Agricultural Production | CAP |
7 | Certificate in Financial Administration | CFA |
DIPLOMA THREE YEARS PROGRAMMES
# | COURSE | CODE |
---|---|---|
1 | Ordinary Diploma in Librarianship | ODLS |
2 | Ordinary Diploma in Animal Health | ODAHP |
3 | Ordinary Diploma in Social Work | ODSW |
4 | Diploma in Pharmaceutical Science | DPS |
DIPLOMA TWO YEARS PROGRAMMES
# | COURSE | CODE |
---|---|---|
1 | Diploma in ICT with Accounting | DICTA |
2 | Diploma in Financial Administration – Accounting | DFAA |
3 | Diploma in Computer Science | DCS |
4 | Diploma in Information Technology | DIT |
5 | Diploma in Social Work | DSW |
6 | Diploma in Journalism | DJ |
7 | Diploma in Agricultural Production | DAP |
8 | Diploma in Librarianship and Information Studies | DLIS |
9 | Diploma in Procurement and Supply Management | DPSM |
10 | Diploma in Hospitality and Tourism Management | DHTM |
11 | Diploma in Heritage Management and Tourism | DHT |
12 | Diploma in Physiotherapy | DPH |
13 | Diploma in Environmental Health Science | DENVH |
DEGREE PROGRAMMES
# | COURSE | CODE |
---|---|---|
1 | Bachelor of Science in Computer Science | BCS |
2 | Bachelor of Arts with Education | BAE |
3 | Bachelor of Arts in History and Archaeology | BAHA |
4 | Bachelor Degree in Banking and Finance | BBF |
5 | Bachelor Degree in ICT with Accounting | BITA |
6 | Bachelor Degree in Accounting and Finance | BAF |
7 | Bachelor Degree in Procurement and Supply Management | BPSM |
8 | Bachelor of Entrepreneurship and Innovation | BEI |
9 | Bachelor of Kiswahili with Education | BAKE |
10 | Bachelor of Arts in Mass Communication | BMC |