The State University Of Zanzibar

SUZA yashiriki kikamilifu Kongamano la Kiswahili la Kimataifa, Havana, Kuba– 8 – 9Novemba, 2024

Kongamano la Kimataifa la Kiswahili limefanyika katika mji wa Havana, nchini Kuba, tarehe 8 na 9 Novemba, 2024. Kongamano hili limehusisha wataalamu na wadau wa Kiswahili kutoka Tanzania na nje ya Tanzania pamoja na wenyeji wa Kuba. Jopo kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) likiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Moh’d Makame Haji, limeshiriki katika kongamano hilo.


Kongamano hilo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri wa Mambo ya Njena Mawaziri wanaosimamia masuala ya utamaduni na michezo pamoja na mabalozi kutoka Tanzania na Kuba.

Kongamano lilifunguliwa rasmi na Mhe. Waziriwa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania, Dkt. Damas Daniel Ndumbaro, kwa niaba ya Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hassan ambae amesisitiza maendeleo ya Kiswahili barani na nje ya Afrika.Takriban washiriki 400 kutoka Afrika, Asia, Amerika na Ulaya wamehudhuria.


Mbali na maendeleo ya lugha, kongamano hilo pia limejumuisha mahusiano mema kati ya Tanzania na Kuba yaliyoanzishwa na waasisiwa mataifa haya mawili, Mwalimu Julius K. Nyererena Fidel Castro. Tamaduni zao na namna mahusiano hayo yatakavyochochea maendeleo ya nchi pia yamejadiliwa kwa kina.

Katika sherehe za ufunguzi wa kongamano hilo, vitabu vitatu vilizinduliwa. Moja wapo ni kitabu cha “Jifunze Kihispania kwa Lughaya Kiswahili”, kilichoandikwa na wahadhiri Dr. Said S. Khamis na Dr.Shani S. Khalfan na kuchapishwa na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar. Kitabu hiki ni miongoni mwa kazi mpya za SUZA zinazotoa maarifa ya usomaji naufundishajiwalughazakigeni. Katika kitabu hiki, maelezo ya kujifunza kihispania yametolewa kwa lugha ya Kiswahili. Uzinduzi wa kitabu hiki unaashiria uwezo wa SUZA kusanifu Kiswahili na kukifanya kuwa lugha ya kufundishia.


Mada zaidi ya ishirini ziliwasilishwa katika kongamano hilo. Miongoni mwa mada zilizowasilishwa ziliandaliwa na wataalamu kutoka. Kwa upande mwengine, SUZA ilitoa mchango wake kupitia wahadhiri na wanafunzi waliotayarisha makala zilizowasilishwa na kuchangiwa katika mijadala iliyofanyika. Mhadhiri Mwadamizi wa Skuli ya Elimuya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, Dr. Maryam Ismail, kwa kushirikiana naProfesa Alwiya Omar, waliwasilisha mada”Mikakati Bora ya Ufundishaji na Ufunzajiwa Lugha ya Kiswahili kwa Wageni” .Mada ambayo imetoa mchango wa mbinu za kisasa za ufundishaji wa lugha ya Kiswahili kwa wageni.
Mbali na wahadhiri kuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha kongamano hilo kwa maandalizi na utoajiwa makala za kitaaluma, Mhe. Riziki Pembe Juma, Waziriwa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ambaye pia ni mwanafunzi wa shahada ya uzamivu ya Kiswahili kutoka Skuli ya Kiswahili na Lugha za Kigeni ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, aliwasilisha makala yake”Mchango wa Wanawake katika Maendeleo ya Kiswahili Duniani: Mifano Kutoka kwa Samia Suluhu Hassan”, akishirikianana Ahmad Y. Sovu.Wasilisho hilo lilijielekeza kuainishana kujadidili mchango wa Raiswa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Samia katika kuimarisha lugha ya Kiswahili na kuitangaza ndani na nje ya mipaka yaAfrika. Ilielezwa kuwa Kiswahili ni lugha pekee ya Afrika inayotambulika ulimwenguni kote kama lugha ya kimataifa.


Mbali na yaliyojiri katika kongamano hilo, Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kimepata fursa ya kufanya mazungumzo na vyuo vikuu mbali mbali vya Kuba kwa lengo la kuanzisha mahusiano ya kitaaluma yatakayo husisha kubadilishana wataalamu na kuongeza ujuzi wa fani mbali mbali.


Jitihada za Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar katika kumataifaisha chuo na kukifanya kuwa cha kimataifa zimeimarishwa kupitia ushiriki wake katika kongamano hili. SUZA imekuwa ikifanya kazi kwa bidii kuongeza kasi ya mashirikiano na taasisi nyingine za kimataifa ili kuboresha elimu na utafiti. Kongamano hili limetoa fursa muhimu kwa SUZA kuonesha uwezo wake wakitaaluma na kuendeleza ushirikiano na vyuo vikuu vya Kuba na taasisi nyingine duniani. Kwa kupitia jitihada hizi, SUZA inakusudia kuongeza ubora wa elimu inayotolewa na kujenga nafasi yake kama chuo kikuu cha kimataifa kinachotoa elimu bora na yenye ushindani.