Skip to main content

The State University Of Zanzibar

MAKAMU MKUU WA CHUO SUZA AUNGANA NA WAFANYAKAZI KUADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Prof. Said Ali Hamad Vuai, ameungana na wafanyakazi wa Chuo hicho katika kuadhimisha kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, kilichofanyika tarehe 9 Oktoba 2026.

Katika maadhimisho hayo, Prof. Vuai alishiriki katika hafla ya kukata na kuwalisha keki wafanyakazi mbalimbali wa SUZA, akiwemo Prof. Abdi Talib Abdalla, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi, pamoja na Prof. Jamal Jumanne Athuman, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Mipango, Fedha na Utawala.

Aidha, hafla hiyo ilihusisha utoaji wa zawadi kwa Maafisa Uhusiano na Masoko wa SUZA kwa kutambua mchango wao katika utekelezaji wa majukumu yao, pamoja na zawadi maalumu kwa Dkt. Khamis Haji Salum, Mkurugenzi wa Shahada za Awali aliyemaliza muda wake.

Maadhimisho hayo yaliandaliwa na Kitengo cha Uhusiano na Masoko cha SUZA kwa lengo la kuimarisha mshikamano miongoni mwa wafanyakazi, kuthamini mchango wao katika utoaji wa huduma na kuendeleza utamaduni wa kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wa Chuo.

Kupitia maadhimisho hayo, SUZA inaendelea kusisitiza umuhimu wa ushirikiano, kuthaminiana na uwajibikaji katika kuhakikisha wateja na wadau wake wanapata huduma bora, kwa wakati na kwa ufanisi.