Skip to main content

The State University Of Zanzibar

SUZA NA MZUMBE ZAJADILI UTEKELEZAJI WA USHIRIKIANO WA KITAALUMA

SUZA NA MZUMBE ZAJADILI UTEKELEZAJI WA USHIRIKIANO WA KITAALUMA

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kupitia Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Said Ali Hamad Vuai, kimekutana na viongozi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe (MU) kwa ajili ya kujadili na kuimarisha utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano wa kitaaluma baina ya taasisi hizo mbili.

Kikao hicho kilifanyika tarehe 27 Septemba 2026 katika Makao Makuu ya SUZA, Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja, ambapo pande hizo mbili zilijadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano yaliyopo katika makubaliano yao.

Miongoni mwa maeneo yaliyojadiliwa ni pamoja na ubadilishanaji wa wafanyakazi na wanafunzi, kufanya tafiti, kuandaa na kufanya mikutano ya kitaaluma pamoja na kutoa huduma za ushauri elekezi.

Ushirikiano huo unalenga kutoa fursa kwa SUZA na Chuo Kikuu cha Mzumbe kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kitaaluma na kitaalamu, huku ukitoa nafasi ya kubadilishana ujuzi, uzoefu na maarifa baina ya taasisi hizo.

Akizungumza katika kikao hicho, uongozi wa SUZA umeendelea kusisitiza umuhimu wa ushirikiano na taasisi nyingine za elimu ya juu katika kuimarisha taaluma, utafiti na huduma za kitaalamu.

Kikao hicho ni sehemu ya juhudi za SUZA na Chuo Kikuu cha Mzumbe kuhakikisha makubaliano ya ushirikiano yanaendelea kutekelezwa kwa manufaa ya taasisi hizo, wafanyakazi, wanafunzi na jamii kwa ujumla.